Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Acts 2 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 When the day of Pentecost arrived, they were all together in one place. Siku ya Pentekoste ilipowadia, waumini wote walikuwa mahali pamoja.
2 Suddenly a sound like a violent, rushing wind came from heaven and filled the entire house where they sat. Ghafula, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali ikatoka mbinguni, ikaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
3 What looked like divided tongues of fire appeared and rested on each one of them. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao.
4 All were filled with the Holy Spirit and began speaking in other tongues, as the Spirit gave them words to say. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
5 At that time devout Jews from every nation under heaven were living in Jerusalem. Basi walikuwako Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.
6 When this sound rang out, a crowd gathered, confused, since each one heard them speak in his own language. Waliposikia sauti hii, umati wa watu walikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
7 They were amazed and astonished, saying, "Are not all these who are speaking Galileans? Wakiwa wameshangaa na kustaajabu, wakauliza, “Je, hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya?
8 How is it, then, that each of us hears them in our own native language? Imekuwaje basi kila mmoja wetu anawasikia wakinena kwa lugha yake ya kuzaliwa?
9 Parthians, Medes, and Elamites; those who live in Mesopotamia, Judea and Cappadocia, Pontus and Asia, Wapathi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto na jimbo la Asia,
10 Phrygia, Pamphylia, Egypt, the parts of Libya near Cyrene; visitors from Rome, Jews and converts to Judaism; Frigia, Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni kutoka Rumi
11 Cretans and Arabs—we hear them telling in our own tongues the mighty works of our Father!" (Wayahudi na wale walioongokea dini ya Kiyahudi), Wakrete na Waarabu: sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.”
12 They were all amazed and perplexed, saying to one another, "What does this mean?" Wakiwa wameshangaa na kufadhaika wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?”
13 But others mocked and said, "They are full of sweet wine." Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa kwa divai!”
14 But Peter stood with the eleven, raised his voice, and declared to them: "Men of Judea, everyone living in Jerusalem—know this and listen carefully to my words. Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akapaza sauti yake na kuhutubia umati ule wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na nyote mnaoishi Yerusalemu, nisikilizeni kwa makini, ili jambo hili lijulikane kwenu.
15 These people are not drunk, as you suppose, for it is only nine o'clock in the morning. Hakika watu hawa hawajalewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi!
16 No, this is what was spoken through the prophet Joel: La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:
17 'And in the last days, says our Father, I will pour out my Spirit on all people; your sons and your daughters will prophesy, your young men will see visions, and your old men will dream dreams. “ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
18 Even on my male servants and my female servants in those days I will pour out my Spirit, and they will prophesy. Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu, nao watatabiri.
19 I will show wonders in the heavens above and signs on the earth below—blood and fire and billows of smoke. Nami nitaonesha maajabu juu mbinguni, na ishara chini duniani: damu, moto, na mawimbi ya moshi.
20 The sun will be turned to darkness and the moon to blood, before the great and glorious day of the Lord comes. Jua litakuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu iliyo tukufu.
21 And everyone who calls on the name of the Lord will be saved.'" Na kila mtu atakayeliitia jina la Mwenyezi Mungu, ataokolewa.’
22 "Men of Israel, hear these words: Jesus of Nazareth—a man our Father attested to you through miracles, wonders, and signs our Father did through him among you, as you yourselves know. “Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo.
23 This man, handed over by our Father's set plan and foreknowledge, you crucified and killed by the hands of lawless men. Baada ya huyu mtu kutolewa kwenu kwa mpango wa Mungu uliokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi mlimuua kwa kumsulubisha msalabani, kwa mikono ya watu waovu.
24 But our Father raised him, freeing him from death's agony, since death could not hold him. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti.
25 For David says of him: 'I saw our Father always before me, for he's at my right hand, so I won't be shaken.' Kwa maana Daudi asema hivi kumhusu: “ ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
26 Therefore my heart was glad and my tongue rejoiced; moreover, my body also will rest in hope. Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika kwa tumaini.
27 For you will not abandon my soul to the grave, nor let your Holy One see decay. Kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.
28 You have shown me the paths of life; you will fill me with gladness in your presence." Umenionesha njia za uzima, utanijaza na furaha mbele zako.’
29 "Brothers, I can tell you plainly: our ancestor David died, was buried, and his tomb remains with us to this day. “Ndugu zangu Waisraeli, nataka niwaambie kwa uhakika kwamba baba yetu wa zamani Daudi alikufa na kuzikwa, nalo kaburi lake lipo hapa hadi leo.
30 Since he was a prophet, he knew our Father had sworn an oath to seat one of his descendants on his throne, Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo, kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha utawala.
31 he foresaw and spoke of the Christ's resurrection, that he was not abandoned to the grave, nor his body saw decay. Daudi, akiona mambo yaliyo mbele, akanena kuhusu kufufuka kwa Al-Masihi, kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu.
32 This Jesus our Father raised up, and we are all witnesses of it. Mungu alimfufua huyu Isa, na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo.
33 So, lifted up to our Father's right hand, having received the promised Holy Spirit from the Father, he poured out what you now see and hear. Basi yeye ametukuzwa hadi mkono wa kuume wa Mungu, na amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu wa Mungu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
34 For David never went up into heaven, but he himself says: "Our Father said to my Lord, 'Sit at my right hand, Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume,
35 until I make your enemies a footstool for your feet.'" hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
36 "So let the whole house of Israel know for certain: our Father made this Jesus, whom you crucified, both Lord and Christ." “Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Isa, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Al-Masihi.”
37 Cut to the heart at this, they asked Peter and the other apostles, "Brothers, what should we do?" Watu waliposikia maneno haya yakawachoma mioyo yao, wakawauliza Petro na wale mitume wengine, “Ndugu zetu tufanye nini?”
38 Peter said to them, "Repent, and each of you be baptized in the name of Jesus Christ for the forgiveness of your sins, and you will receive the gift of the Holy Spirit. Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mungu.
39 For the promise is for you, your children, and all far off—as many as the Sovereign our Father will call to himself." Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.”
40 And with many other words he warned and urged them, saying, "Save yourselves from this corrupt generation." Petro akawaonya kwa maneno mengine mengi na kuwasihi akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kilichopotoka.”
41 So those who welcomed his message were baptized, and about 3,000 people were added that day. Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa, na siku ile waliongezeka watu wapatao elfu tatu.
42 They devoted themselves to the apostles' teaching and deep communion, to the breaking of bread and the prayers. Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali.
43 Awe came over everyone, and many wonders and signs were done through the apostles. Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume.
44 All who believed were together and had all things in common. Waumini wote walikuwa mahali pamoja, nao wakashirikiana katika mambo yote.
45 They sold their property and possessions and distributed the proceeds to all, as anyone needed. Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.
46 Every day, devoting themselves together in the temple, breaking bread house to house, they shared food with joyful, sincere hearts, Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe,
47 praising our Father, with favor among all the people. The Lord added to their number daily those being saved. wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]