Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

3 John 1 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 The elder, to the beloved Gaius, whom I love in truth. Mzee. Kwa Gayo rafiki yangu nimpendaye katika kweli.
2 Beloved, I pray you prosper in every way and stay healthy, as your soul prospers. Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.
3 I rejoiced greatly when brothers arrived and testified about your faithfulness to the truth—for you truly are walking in it. Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza kuhusu uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli.
4 I have no greater joy than this: to hear that my children are walking in the truth. Sina furaha kubwa kuliko hii, ya kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.
5 Beloved, you act faithfully in all you do for the brothers, even strangers. Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako.
6 They testified to your love before the church. Send them on in a way worthy of our Father. Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya jumuiya ya waumini. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu.
7 For they went out for the sake of the Name, accepting nothing from the Gentiles. Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasiomwamini Al-Masihi.
8 Therefore we ought to support such people, so that we may be fellow workers for the truth. Kwa hiyo imetupasa sisi kuonesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli.
9 I wrote something to the church, but Diotrephes, who loves being first among them, does not receive us. Nililiandikia kundi la waumini, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu.
10 So if I come, I'll expose what he's doing—slandering us with malicious words. Not satisfied with that, he refuses to welcome the brothers, stops those who want to, and throws them out of the church. Hivyo nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa waumini.
11 Beloved, don't imitate evil, but good. Whoever does good is from our Father; whoever does evil hasn't seen our Father. Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema anatoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.
12 All speak well of Demetrius, and so does the truth. We testify too, and you know our testimony is true. Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli.
13 I had much to write to you, but I would rather not write with pen and ink. Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino.
14 I hope to see you soon, and we will talk face to face. Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana.
15 Peace to you. The friends send their greetings. Greet each of the friends by name. Amani iwe kwako. Rafiki zetu walio hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walio huko, kila mmoja kwa jina lake.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]