Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

2 Chronicles 8 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 After twenty years, in which Solomon built the house of our Father and his own palace, Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alilijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba lake mwenyewe la kifalme,
2 Solomon rebuilt the cities that Huram had given him, and settled the people of Israel in them. Sulemani akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo.
3 Then Solomon marched against Hamath-zobah and overpowered it. Kisha Sulemani akaenda Hamath-Soba na kuuteka.
4 He built Tadmor in the wilderness, along with all the storage cities he built in Hamath. Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa, na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi.
5 He also rebuilt Upper Beth-horon and Lower Beth-horon as fortified cities, with walls, gates, and bars, Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo.
6 Baalath, all Solomon's supply cities, his chariot and horsemen cities, and all he desired to build in Jerusalem, Lebanon, and his whole realm. Sulemani pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.
7 There were still people left from the Hittites, Amorites, Perizzites, Hivites, and Jebusites, who were not Israelites. Watu wote waliosalia kutoka kwa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (haya mataifa hayakuwa Waisraeli),
8 Their descendants still living in the land, whom Israel had not destroyed, Solomon conscripted for forced labor, as they still are today. yaani wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwa wamewaangamiza: hawa Sulemani akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo.
9 Solomon enslaved no Israelites for his work; they were soldiers, commanders of his officers, and commanders of his chariots and horsemen. Lakini Sulemani hakuwafanya Waisraeli watumwa kwa ajili ya kazi yake; hao ndio walikuwa wapiganaji wake, majemadari wake, maafisa wake, majemadari wa magari yake ya vita, na wapanda farasi wake.
10 These were King Solomon's chief officers: 250 who supervised the people. Pia walikuwa maafisa wakuu wa Mfalme Sulemani, maafisa wakaguzi mia mbili na hamsini waliosimamia watu.
11 Solomon brought Pharaoh's daughter from the City of David to the house he built her, saying, "No wife of mine will live in David king of Israel's house, for holy is wherever our Father's ark has entered." Sulemani akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la Mwenyezi Mungu limefika ni patakatifu.”
12 Then Solomon offered burnt offerings to our Father on the altar he built before the portico, Mfalme Sulemani akamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu ambayo alikuwa ameijenga mbele ya ukumbi,
13 daily as required, by Moses' command: Sabbaths, New Moons, and three yearly festivals—the Feast of Unleavened Bread, the Feast of Weeks, and the Feast of Tabernacles. kulingana na mahitaji ya kila siku kwa ajili ya sadaka zilizoamriwa na Musa kwa ajili ya Sabato, Mwezi Mwandamo na sikukuu nyingine tatu za mwaka: Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma na Sikukuu ya Vibanda.
14 Following his father David's rules, he set priestly divisions for service, Levite divisions to praise and serve before the priests as each day required, and gatekeeper divisions at each gate, for David the man of our Father had commanded it. Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hivi ndivyo Daudi mtu wa Mungu alivyokuwa ameagiza.
15 They followed the king's orders to the priests and Levites exactly, down to the storerooms. Nao hawakuziacha amri za mfalme alizoamuru makuhani au Walawi katika jambo lolote, ikiwa ni pamoja na zile za hazina.
16 All Solomon's work was finished, from the day our Father's house was founded until its completion; our Father's house was complete. Kazi yote ya Mfalme Sulemani ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu ulipowekwa hadi kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la Mwenyezi Mungu likamalizika kujengwa.
17 Then Solomon went to Ezion-geber and Eloth on the seacoast in the land of Edom. Ndipo Sulemani akaenda Esion-Geberi na Elathi katika pwani ya Edomu.
18 Huram sent him ships by his servants, with sailors who knew the sea; they sailed with Solomon's servants to Ophir, took about seventeen tons of gold, and brought it to King Solomon. Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Sulemani wakasafiri kwa bahari hadi Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]