Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

2 Chronicles 17 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 His son Jehoshaphat became king in his place and strengthened himself against Israel. Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake na akajiimarisha dhidi ya Israeli.
2 He stationed troops in all Judah's fortified cities and garrisons in the land of Judah and in the cities of Ephraim that his father Asa had captured. Akaweka jeshi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, na kuweka askari walinzi katika Yuda na katika miji ya Efraimu ambayo baba yake Asa alikuwa ameiteka.
3 Our Father was with Jehoshaphat, for he walked his father David's earlier ways, not seeking the Baals. Mwenyezi Mungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali
4 Instead, he sought the Father his father served, obeyed his commandments, and not the practices of Israel. bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za Waisraeli.
5 So our Father secured the kingdom in his hand; all Judah brought gifts to Jehoshaphat, and he had great wealth and honor. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima.
6 His heart was devoted to our Father's ways; he removed the high places and Asherah poles from Judah. Moyo wake ukawa hodari katika njia za Mwenyezi Mungu na zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia na nguzo za Maashera katika Yuda.
7 In his reign's third year he sent his officials Ben-hail, Obadiah, Zechariah, Nethanel, and Micaiah to teach in Judah's cities, Katika mwaka wa tatu wa utawala wake Yehoshafati, alituma maafisa wake ambao ni Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda.
8 and the Levites with them: Shemaiah, Nethaniah, Zebadiah, Asahel, Shemiramoth, Jehonathan, Adonijah, Tobijah, Tob-adonijah; and with them the priests Elishama, Jehoram. Pamoja nao walikuwa na Walawi kadhaa: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, Tob-Adonia; na pamoja nao makuhani Elishama na Yehoramu.
9 They taught throughout Judah, carrying the Book of our Father's Instruction, going to all Judah's cities, teaching the people. Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu; wakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu.
10 The dread of our Father fell on all the kingdoms around Judah, so they made no war on Jehoshaphat. Kicho cha Mwenyezi Mungu kikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati.
11 Some Philistines brought Jehoshaphat gifts and silver tribute; the Arabs brought flocks: 7,700 rams, 7,700 male goats. Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi na fedha kama ushuru, nao Waarabu wakamletea mifugo: kondoo dume elfu saba na mia saba, na mbuzi elfu saba na mia saba.
12 Jehoshaphat grew more and more powerful, and he built fortresses and storage cities in Judah. Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda,
13 He had large supplies in the cities of Judah, and mighty warriors in Jerusalem. na akawa na vifaa vingi katika miji ya Yuda. Pia aliweka wapiganaji wenye uzoefu huko Yerusalemu.
14 Their enrollment by ancestral house: from Judah, commanders of thousands—Adnah the commander, with him 300,000 mighty warriors; Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: Jemadari Adna akiwa na wapiganaji elfu mia tatu;
15 next to him was Jehohanan the commander, and with him 280,000; aliyefuata ni jemadari Yehohanani, akiwa na wapiganaji elfu mia mbili na themanini;
16 next Amasiah son of Zichri, who volunteered for our Father, with him 200,000 mighty warriors. aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi ya Mwenyezi Mungu, akiwa na wapiganaji elfu mia mbili.
17 From Benjamin: Eliada, a mighty warrior, and with him 200,000 armed with bow and shield; Kutoka Benyamini: Eliada, mpiganaji hodari, akiwa na watu elfu mia mbili wenye nyuta na ngao;
18 next to him Jehozabad, and with him 180,000 equipped for war. aliyefuata ni Yehozabadi, akiwa na wapiganaji elfu mia moja na themanini tayari kwa vita.
19 These men served the king, besides those he stationed in the fortified cities throughout Judah. Hawa ndio wapiganaji waliomtumikia mfalme, mbali na ambao mfalme aliwaweka katika miji yenye ngome katika Yuda yote.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]